Dereva Daraja La II
Job Description
1.1 SIFA ZA KUAJIRIWA
Kuajiriwa wenye cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja E au C ya
uendeshaji magari ambayo wamefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila
kusababisha ajali pamoja na vyeti vya mafunzo vilivyowapatia sifa ya kupata madaraja
husika. Wawe wamehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji magari (Basic Driving
Course) yanayotolewa na Chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
1.1.1 MAJUKUMU NA KAZI
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalilmbali kwenye safari za kikazi;
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
vi. Kufanya usafi wa gari; na
vii. Kufanya kazi zingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.
1
1.1.2 NGAZI YA MSHAHARA
TGS B
1.2 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II - NAFASI MOJA (1)
1.2.1 SIFA ZA KUAJIRIWA
Kuajiriwa mwenye elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) pamoja na
Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya uhazili kutoka chuo
chochote kinachotambuliwa na Serikali. Aidha, awe amefaulu somo la Hatimkato ya
Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na awe amepata mafunzo ya
programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint, Internet, Email na
Publisher.
1.2.2 MAJUKUMU NA KAZI.
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida;
ii. Kusaidia kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao
na kuwaelekeza sehemu wanazoweza kushughulikiwa;
iii. Kusaidia kutunza taarifa / kumbukumbu za Matukio, Miadi, Wageni, tarehe
za vikao, Safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine zilipangwa
kutekelezwa
iv. katika Ofisi anayofanyia kazi na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati
unaohitajika;
v. Kusaidia kutatua na kumpatia Mkuu wake majalada, nyaraka au
kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo Ofisini;
vi. Kusaidia kufikisha maelezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi
wake na kumtaarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na
wasaidizi hao;
vii. Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa maofisa walio katika
sehemu alipo na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu
zinazohusika; na
viii. Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa
kazi.
1.2.3 NGAZI YA MSHAHARA
TGS C
2
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
i. Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na
usiozidi miaka 45.
Log in to read the full job — and 763 more open right now
You are reading the opening of this advert. An account is free and opens the rest of it, including the requirements and exactly how to apply before the deadline.
- The complete description, requirements and how to apply
- Build a professional CV aimed at this exact role
- Link your WhatsApp and get every morning’s new jobs sent to you
How to Apply
The employer’s application route — the email, portal or form, and the deadline — opens as soon as you have a free account.
Create a free account or log in